Kwa wiki moja, jifurahishe pamoja na watu wema pa mahali pazuri!

Ni likizo kupita likizo lolote ulilojua. Watu kutoka mataifa mbali mbali wanajuana porini. Sikia wale walioenda Crazy Camps.

Kila wiki ina michezo yake. Kwa mfano, kwa Crazy Mountain Camps, watu wanapanda mlima pamoja. Kwa Crazy Snow Camps, watu wanacheza michezo za theluji (ski, snowboard). Na kuna mandhari ingine pia.

Na bora ya michezo ni watu ambao unakutana. Unapoanza wiki, huwajui. Kwa wiki, unapika pamoja, unakula pamoja, unasafisha pamoja, unacheza na kufanya michezo pamoja. Mwishowe, umepata marafiki wengi wapya. Umejifunza mambo mapya kuhusu kila mtu, na kuhusu wewe mwenyewe pia.

Crazy Snow Camp

Kama una miaka 18 au juu, tunakukaribisha. Wale ambao wameisha fanya Kambi ya Raha walikuwa nusu-nusu wanawake na wanaume. Kwa wastani, walikuwa na umri 33, (mdogo wa yote alikuwa na umri 19, mzee alikuwa na umri 56). 68% hawana mme au mke, 24% wameowa lakini mke/mume wake hawakufika nao, 8% walikuja na mke/mume wao. Hawa walitoka nchi 31 na bara 4. 44% hawakai kwa taifa yao kwa sasa.

Kwa kawaida, watu wanaongeana kwa kingereza, lakini kingereza si luga ya mama kwa watu wengi. Kwa hiyo, kama unafahamu kingereza kidogo tu, hakuna shida.

Mara kwa mara tunaongeza mandhari na mahali ya kambi. Jiunga kwa website yetu kama unataka tukujulishe kuhusu mambo mapya ya Crazy Camps.

Crazy Camps siyo kampuni au shirika. Ni mimi tu, na tengeneza hiyo Kambi kwa sababu na furahi sana kuifanya. Ninaamini kwamba hata wewe utajifurahia na Crazy Camps!